HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Samuel Kosgei
WAWAKILISHI wadi kaunti ya Marsabit walijiunga na wenzao kote nchini kugoma kwa kususia majukumu yao kama MCAs baada ya serikali kupuuza malalamishi yao kadhaa ikiwemo nyongeza ya mishahara na kunyimwa hazina ya wadi.
Kiongozi wa wengi katika bunge la Marsabit Bernard Leakono akizungumza na Shajara ya Jangwani kwa njia ya simu alisema kuwa watasusia kazi hadi tarehe 8 mwezi wa nane hadi kilio chao kitakaposikika.
Anasema baadhi ya malalamishi yao ni pamoja na kutaka MCAs wateule kupewa pesa za maendeleo na pia sekta ya afya isichukuliwe na serikali ya kitaifa.
Leakono ambaye pia ni mwakilishi wadi wa Loglogo alishikilia kuwa lazima serikali isikie kilio chao kabla ya wao kurejea kazini.
Alisema kwa muda MCAs wamekosewa heshima yao hivyo kutaka maslahi yao yaangaziwe kabla ya kupitisha bajeti ya kaunti.