KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Silvio Nangori,
Seneta wa kaunti ya Marsabit Muhamud Chute ametoa wito kwa idara ya usalama kuwakamata wanaoshukiwa kuhusika katika wizi wa chakula unaodaiwa kufanyika katika eneo la sololo eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii moja kwa moja Seneta Chute amesema kwamba ni aibu zaidi kushuhudiwa wizi wa chakula cha msaada wakati ambapo wananchi wanapitia changamoto ya baa la njaa.
Amesema kwamba yuko tayari kufikisha swala hilo kwa Rais William Ruto ili wanaoshukiwa wakumbane na mkono wa sheria na chakula hiyo kurejeshwa kwa wananchi.
Kauli yake inajiri siku moja baada ya DCC wa Sololo Robert Nzuki kutaja kwaba tayari uchunzi umeanzishwa ili kuwatia baroni wahusika katima kisa hicho ambapo zaidi ya magunia 117 ya chakula cha msaada kilichopaniwa kupewa wananchi wanaoadhirika na janga la baa la njaa katika eneo hilo kilipotea kwa njia isiyoeleweka.