WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Isaac Waihenya
Tayari kaunti ndogo tano katika kaunti ya Marsabit ambazo ni Marsabit Central, Sololo, Loyangalani, Turbi/Bubisa na Chalbi zimekamilisha zoezi la ukaguzi wa shule za msingi, za kibinafsi na za umaa kuhusiana na uwezo wa shule hizo kuwa na shule za upili ngazi ya chini Junior Secondary.
Kufikia sasa jumla ya shule 120 za umaa na za kibinafsi zimetajwa kuwa na uwezo huo.
Kwa mujibu wa msimamizi wa kiwango cha ubora wa elimu katika kaunti ya Marsabit Mumas Wanyama ni kuwa zoezi hilo linatarajiwa kukamilika kufikia mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake, Wanyama ametaja kwamba tayari shule 22 jimboni zimebainika kuwa na uwezo wa kuwandaa wanafunzi hadi gredi ya sita ambazo zitajulikana kama Feeder Schools ila wanafunzi watahitajika kujiunga na shule nyingine katika kiwango cha gredi ya saba (Junior Secondary).
Aidha wanyama amewarai wazazi kuhakikisha kwamba wanao waliofanya mtihani wa kitaifa wa gredi ya 6 wanajiunga na Junior Secondary kwani watakaokaidi hilo wakabiliwa kisheria.