HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya,
Jumla ya shule 196 za umaa na za kibinafsi katika kaunti ya Marsabit zimetajwa kuwa na uwezo kuwa na shule za upili ngazi ya chini Junior Secondary.
Kwa mujibu wa msimamizi wa kiwango cha ubora wa elimu katika kaunti ya Marsabit Mumas Wanyama ni kuwa idadi hiyo inajumlisha shule 149 za umaa pamoja na 47 za kibinafsi baada ya shule 225 kupigwa msasa huku zile za kibinafsi ambazo hazikuwa na vigezo hitajika zikitarajiwa kufungwa.
Wanyama ameyataja hayo baada ya idara ya elimu kaunti ya Marsabit kukamilisha zoezi la ukaguzi wa shule za msingi, za kibinafsi na za umaa kubaini iwapo zina uwezo wa kuwa na shule za upili ngazi ya chini Junior Secondary.
Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake, Wanyama ametaja kwamba tayari shule 19 jimboni zimebainika kuwa na uwezo wa kuwandaa wanafunzi hadi gredi ya sita ambazo zitajulikana kama Feeder Schools ila wanafunzi watahitajika kujiunga na shule nyingine katika kiwango cha gredi ya saba (Junior Secondary).
Aidha Wanyama ametaja kwamba ni shule mbili pekee ambao ni Little Angle Acadamy hapa mjini Marsabit pamoja na Jamia academy mjini moyale ambazo zimewaza kujenga shule ya Junior secondary na kuwa kando na shule ya msingi.
Mkuu huyo wa elimu jimboni amewarai wazazi kuhakikisha kwamba wanao waliofanya mtihani wa kitaifa wa gredi ya 6 wanajiunga na Junior Secondary kwani watakaokaidi hilo wakabiliwa kisheria.