County Updates

Bunge la Marsabit Lamhoji Wario Boru Kuwa Mwenyekiti wa Manispaa ya Mji wa Marsabit

Wanachama wa Kamati ya Ardhi na Ukuaji Miji katika bunge la Marsabit
Na Samuel Kosgei
BUNGE la kaunti ya Marsabit imemhoji Wario Boru ambaye alipendekezwa na gavana Mohamud Ali kuwa mwenyekiti wa Manispaa ya Marsabit baada ya nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda sasa.
Iwapo kamati hiyo ya bunge itamwidhinisha basi Wario atatwaa nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa Roba Sereka ambaye alitoweka mapema mwaka jana.
Wario alikuwa akiwania ubunge eneobunge la Saku mwaka jana kwa tiketi ya chama cha UDM ila alibwagwa na mbunge wa sasa Dido Raso.
Kamati ya Ardhi na Ukuaji Miji katika bunge la Marsabit ndiyo iliyomhoji ikiongozwa na MCA wa Marsabit central Jack Elisha.

Subscribe to eNewsletter