IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Waihenya Isaac,
Zaidi ya aslimia 90 ya wakaazi wa kaunti ya Marsabit wameadhirika na matatizo ya afya ya akili.
Hayo ni kwa mujibu wa mwanasaikologia katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Victor Karani.
Akizungumza na Idha hii kwa njia ya kipekee, Karani ametaja kuwa maswala ya Ukosefu wa Usalama, na hali ngumu ya maisha kama maswala yaliyochangia kuongezeka kwa idadi hii.
Ametaja kuwa idadi kubwa ya wananchi wanaadhirika pasi na wao kujua jambo linalochangia idadi hii kuzidi kuongezeka kila kukicha.
Aidha Karani ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kuchunguza hali yao ya afya ya kiakili iwapo watashuhudia swala la msongo wa mawazo.
Mtaalamu huyo wa ushauri nasaha amewataka wananchi kutumia mbinu za kuzungumzia matatizo yao kuliko kuamua kujitoa uhai.