HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Samson Guyo,
Baada ya Mamlaka ya kudhibiti kawi nchini EPRA kutangaza kuongezeka kwa bei ya mafuta mapema wiki hii, wakaazi mjini marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na hilo.
Wakizungumza na Radio Jangwani baadhi ya wakaazi wakiwemo walio katika sekta ya uchukuzi pamoja na wale wamiliki wa magari na pikipiki wameelezea kusikitishwa kwao,wakitaja kutelekezwa na serikali.
Wameelezea kuwa huenda bei ya nauli ikaongezeka kufuatia hatua hiyo.
Katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, bei hizo zimesalia kuwa zile zile licha ya kupanda kwa bidhaa katika soko la kimataifa.
Ila kwa sasa lita moja ya petrol inauzwa kwa shilingi 129.72 dizeli ikiuzwa kwa 110.6 na mafuta Taa yakiuzwa kwa shilingi 103.54.