HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya,
Kaunti ya Marsabit imeongezewa kauti ndogo 4 zaidi na kuifainya kuwa na jumla ya kaunti ndogo kuwa 13.
Kupitia gazeti rasmi la serekali, wizara ya usalama wa ndani imeziongeza kaunti ndogo za Korr makao yake makuu yakiwa ni Korr, Sagante/Jaldesa, Uran na kaunti ndogo ya Golbo ambayo makao yake makuu yatakuwa eneo la Godoma
Aidha kaunti ndogo ya Laisamis imeongezewa kata kadhaa zikiwemo Hafare, kata ya Halisurwa na Mpagas.
Vilevile kaunti ndogo hiyo imepata kata ndogo 6 zaidi ambazo ni Korr Magharibi, na Korr Mashariki, kata ndogo ya Buuri Urween, Burrasidakhan,Lependera na kata ndogo ya Dadabo Hagudhan.
Kadhalika kaunti ndogo ya Moyale imepata divisheni mbili zaidi ambao ni Nanaw na Bori.
Aidha kaunti ndogo hiyo imeongezewa kata tatu zaidi ambazo ni Qoqom Central, Biashara Street na Godoma Didiqo huku kata ndogo tano zaidi zikibuniwa ambazo ni pamoja na Qoqom 1 na Qoqom 2,Biashara street, Bururi na kata ndogo ya Garse.