WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Grace Gumato,
Jumla ya mifugo 224,000 wameangamia kutokana na makali ya ukame katika kaunti ya Marsabit tangu mwaka wa 2021.
Kwa mijibu wa Henry Mustafa ambaye ni mkurungezi wa mamlaka ya kukabiliana na majanga kaunti Marsabit NDMA, Kondoo na mbuzi 30,000 wameweza kuangamia katika kaunti ndogo ya Noth Horr.
Mustafa amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamechangia pakubwa kuwepo kwa makali ya ukame katika kaunti ya Marsabit.
Aidha amesema kuwa wafugaji hapa jimboni wamegeukia ufugaji wa Ngamia kwa wingi kwani ndio wanaoweza kustahimili makali ya ukame huku Ngombe wakitajwa kupungua.
Hata hivyo Mustafa amesema kwamba kumekuwa na changamoto kubwa wakati huu wa ukame ikiwemo utapiamlo, ukosefu wa chakula na maji na pia wanyama kufa kutokana na ukosefu wa malisho.