HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya,
Gavana wa Marsabit Mohamud Ali ametangaza kuwa jamii ya Borana kwa kauli mmoja imekubaliana kuachia nafasi zingine za uongozi kwa jamii zingine na kuwania nafasi ya Ugavana pekee.
Gavana Ali amesema kuwa jamii hiyo itafanaya kazi na jamii zingine katika kaunti hii na kuzipa nafasi ya kuwa uongozini haswa katika wadhifa wa Useneta na ule wa mwakilishi wa kike.
Ameyasema hayo alipokutana na makundi mbali mbali ya akina mama, vijana pamoja na wazee kutoka eneo bunge la Saku nyumbani kwake.
Wakti uo huo Gavana Ali amewarai wananchi jimboni kudumisha Amani wakti huu wa kampeni huku akimshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kile amekitaja kuwa ni ‘kuheshimu ombi lake’ la kuundwa kwa kaunti ndogo nne zaidi katika kaunti ya Marsabit.
Amesema kuwa kaunti ndogo hizo nne zitahakikisha maendeleo na raslimali zipo karibu na mwananchi.
Amewataka wananchi hapa jimboni kuunga mkono chama cha UDM pamoja na vuguvugu la Azimo la Umoja ambavyoa amevitaja kuwa ndivyo vitakavyounda serekali ijayo.