County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Zaidi Ya Vijana 2,000 Katika Kaunti Ya Marsabit Walijitokeza Kwenye Zoezi La Kusajiliwa Kama Vibarua Katika Shirika La Huduma Kwa Wanyamapori Nchini KWS.

Vijana Wakti Wa Zoezi La Kusajiliwa Kama Vibarua Katika Shirika La Huduma Kwa Wanyamapori Nchini KWS.
Picha Hisani.

By Mark Dida,

Zaidi Ya Vijana 2,000 Katika Kaunti Ya Marsabit Walijitokeza Kwenye Zoezi La Kusajiliwa Kama Vibarua Katika Shirika La Huduma Kwa Wanyamapori Nchini KWS.

Naibu Mkurugenzi Mkuu Wa KWS Kaunti Ya Marsabit Robert Obrein Amesema Wamesajili Vijana 93 Kutoka Kaunti Zote Ndogo Jimboni Kati Ya Vijana Zaidi Ya 2,000 Walijitokeza Kushiriki Zoezi Hilo.

Obrein Amesema Vibarua Hao Waliosajiliwa Na Shirika Hilo Jana Watasaidia Kulinda Hifadhi Za Wanyamapori Na Misitu Ya Kaunti Zote 47 Nchini, Akisema Serikali Imetenga Fedha Kusimamia Mpango Huo.

Obren Amesema Baadhi Ya Vijana Waliotuma Maombi Ya Kazi Hiyo Ya Kandarasi Hawakushiriki Kwani Walirejea Shuleni Baada Ya Kufunguliwa.

Kwa Upande Wao Vijana Waliojitokezza Kushiriki Zoezi Hilo Mjini Marsabit Wamepongeza KWS Kwa Kuendesha Zoezi Hilo Kwa Uwazi. Vibarua Waliochukuliwa Watahudumu Kwa Miezi Sita Pekee Na Kisha Wengine Kupewa Nafasi Sawa Na Hiyo.

 

 

Subscribe to eNewsletter