KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Picha;Radio Jangwani
By Grace Gumato,
Wanaume watano wamefikishwa kizimbani katika mahakama ya Marsabit kwa makosa ya wizi kinyume cha sheria kwenye kesi mbili tofauti.
Ramadhan Halkano, Diba Golicha, Abdi Hirbo na Hussein Yussuf walikamatwa jana Jumanne ambapo wameshtakiwa kwa makosa ya kumuibia mfanyibiashara Isacko Orto mashine ya kusaga nyasi ya ng’ombe, milango tatu ya chuma na moja ya mbao yote yenye dhamani jumla ya shilingi 105,800.
Washukiwa walifikishwa mbele ya hakimu Tom Mbayaki Wafula ambapo walikana kuhusika kufanya uhalifu huo katika Dirib Gombo, eneo bunge la Saku.
Hakimu amewaagiza kubaki rumande hadi kesi yao itakaposkizwa tena Jumatatu juma lijalo.
Wakati uo huo Hussein Boru alifikishwa mbele ya mahakama iyo hiyo kwa tuhuma ya kuvunja duka la Mohammed Diba Boru na kuiba simu haina ya oppo na machine ya kusaga nyama.
Boru ameshtakiwa kuiba vifaa hivyo vinavyogharimu jumla ya shilingi 21,000 katika mtaa wa Manyatta Otte hapa mjini Marsabit.
Alikifishwa mbele ya hakimu Tom Mbayaki Wafula na kukana mashtaka dhidi yake.
Mshukiwa atakabaki rumande kusubiri kusikizwa tena kwa kesi yake kesho Alhamisi.