County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Visa vya talaka kati ya wanandoa wa jamii zinazoishi katika kaunti ya Marsabit viongezeka. – Asema Kadhi Mkuu wa Mahakama ya Marsabit Ibrahim Tullu.

 

Kadhi Mkuu wa Mahakama ya Marsabit Ibrahim Tullu.
Picha; Samuel Kosgei

By Samuel Kosgei,

Kadhi Mkuu wa Mahakama ya Marsabit Ibrahim Tullu ameonesha masikitiko yako kutokana na ongezeko la visa vya talaka kati ya wanandoa wa jamii zinazoishi jimbo hili.

Kadhi Tullu akisema na shajara ya jangwani amekiri kuwa tangu ajiunge na idara ya mahakama ktk kaunti ya Marsabit September 2019, visa 120 vya talaka vimewasilishwa kwake.

Kwa mwezi mmoja anasema kuwa anapata visa kati ya 16-20 vya talaka katika mahakama yake.

Ameendelea kusema kuwa wengi wa wanaowasilisha kesi za talaka ni vijana matineja wadogo wanaojiingiza kwenye ndoa kiholela suala ambalo anasema kuwa limechangiwa na matumizi ya dawa za kulevya na shinikizo la rika.

Kadhi Mkuu wa Mahakama ya Marsabit Ibrahim Tullu.
Picha; Samuel Kosgei

Aidha amelaumu wazee kidini kwa kuibuka na kauli ya kupunguza pesa za kulipia mahari hadi shilingi elfu 10k akisema kuwa ndio sababu moja wapo kuu inayosababisha hali hiyo. Ameonya wazazi kutoruhusu watoto wao kuoa au kuolewa wakiwa wangali wadogo kwa wengi wao bado hawajakomaa kiakili.

Subscribe to eNewsletter