IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
By Waihenya Isaac,
Viongozi wa kidini nchini wametakiwa kuwa Katika mstari wa mbele katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mchakato wa BBI.
Kwa Mujibu wa Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Mombasa Askofu mkuu Martin Kivuva ni kuwa ni jukumu la kila kiongozi wa kidini kuelimisha waumini wake kuhusiana ripoti hiyo ili kufahamu kilichomo kabla ya kufanya maamuzi ya kuipinga au kuiunga mkono.
Askofu Kivuva amewahimiza viongozi wote wa kidini kuelezea kwa kina manufaa ya BBI na vipengee ambavyo vinapaswa kufanyiwa marekebisho ya kura ya maamuzi.
Aidha amewataka viongozi wa kisiasa nchini kuhubiri amani na sio kuwagawanya Wakenya katika mirengo ya kisiasa.