County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Utafunaji Mwingi Wa Miraa Wafanya Vijana Kukatiliwa Jeshi, Sakuu

Picha;Hisani

By Adano Sharawe,

Makurutu wengi waliojitokeza kutafuta nafasi ya kusajiliwa kwenye kikosi cha jeshi la Kenya (KDF) eneo la Saku hii leo walitemwa nje kutokana na matokeo ya vipimo vyao kuwa na chembechembe za mihadarati hasa miraa.

Afisa msimamizi wa shughuli ya usajili wa makurutu kuingia jeshini eneo la Saku, Luteni Kanali Martin MalukI pia aliambia wanahabari kuwa idadi kubwa ya makurutu walitemwa kutokana na uzani hafifu wa mwili uliohitajika.

Amewasihi wazazi na utawala wa kaunti ya Marsabit kutoa hamasa kwa vijana wajiepushe na utafunaji mwingi wa miraa unaoharibu meno na kupunguza nafasi yao ya kujiunga na KDF.

Subscribe to eNewsletter