HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
By Jillo Dida Jillo
Kaunti ya Marsabit imeungana na wakenya wengine kusheherekea juhudi zake za kukabiliana na ugonjwa wa saratani huku Ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya saratani hii leo -kauli mbiu wa mwaka huu ikiwa ni ushirikiano kati ya wagonjwa na wahudumu katika kukabili saratani hapa nchini.
Maadhimisho ya leo yamefanyika kupitia mitandao ya kijamii kutokana na Jinamizi la corona.
Saratani ni ugonjwa wa Uvimbe inyosababishwa na Vitu kama vile virusi, bakteria, parasiti, madini mazito kwa mfano asbestos pamoja na mionzi.
Dkt Adano Diba Kochi ni mkurungezi wa afya katika serikali ya kaunti ya Marsabit amekeri kuwepo na changamoto katika kukabiliana na Saratani hapa jimboni.
Aidha Kochi amehaidi kuongeza jitihada katika kuamsha ari na hamasa ya wananchi kupima Saratani ili kujua hali zao sambamba na Kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani katika maeneo ya vijijini kwa kuimarisha huduma za matibabu ya Saratani yaani matibabu kwa njia ya Dawa (Chemotherapy) na matibabu kwa njia ya mionzi (Radiotherapy) katika Hospitali za Rufaa za Marsabit na kalacha.
Dkt Kochi amebaini kuwa Ugonjwa wa saratani unasabishwa na Vyanzo ambavyo ni pamoja na mtindo wa kimaisha yaani (Life Style) kama vile uvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula usiofaa matumizi ya pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya na kutofanya mazoezi.
Katika maadhimisho ya leo Dkt Kochi ametolea wito wakaazi kuripoti kisa chochote kabla ya kukidhiri.
Ugonjwa wa Saratani huanza pale seli za mwili zinapokuwa bila mpangilio na kusababisha uvimbe, na huweza kusambaa sehemu mbali mbali za mwili.
Kulingana na Kochi Saratani huanza taratibu bila maumivu yeyote na huchukua muda kabla ya kuonesha dalili.
Ikumbukwe Siku ya wagonjwa wa SARATANI hushejerekewa kote ulimwenguni kila mwaka rarehe 4 mwezi Februari.