Wanafunzi 19 kati ya 20 kutoka shule ya upili ya Ngurnit kujiunga na vyuo vikuu.
January 10, 2025
Na Emmanuel Amalo,
Mwenyekiti wa chama cha wauza nyama-Butcher Sacco eneo hili, Diba Galgallo amesema kuwa wanapitia changamoto si haba kutokana na machafuko ya kila mara katika eneo hili.
Galgallo amedokeza kuwa biashara hiyo huathirika vibaya kila mara kunapotokea mapigano ya kikabila ikizingatiwa kichinjio kikuu kiko nje kidogo ya mji wa Marsabit na huwa vigumu kusafirisha nyama kutoka eneo hilo hadi mjini humu kutokana na hofu ya mashambulizi.
Kulingana na Diba wafanyibiashara wengi wanategemea kuuza nyama kujikimu-ambayo kwa sasa anadai ni vigumu kupatikana.
Aidha ametoa wito kwa serikali kuingilia kati kwa kuwahakikishia usalama wao ili waweze kuendesha shughuli zao bila ya uoga wowote.