County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Tume Ya Uiano Na Utengamano Nchini NCIC Inangangana kuwarejesha viongozi wa kaunti ya Marsabit Katika meza ya mazungumzo baada ya mazungumzo ya hapo awali kusabaratika.

Kamishina Wa NCIC Denvas Makori.
Picha;Hisani.

By Waihenya Isaac,

Tume Ya Uiano Na Utengamano Nchini NCIC Inangangana kuwarejesha viongozi wa jimbo hili Katika meza ya mazungumzo baada ya mazungumzo ya hapo awali kutawanyika.

Hayo ni kwa mujibu wa kamishna wa tume hiyo Denvas Makori.

Akizungumza na Idhaa hii kwa njia ya simu, Makori ametaja swala la kubuniwa kwa wilaya mbili zaidi katika kaunti ndogo ya North Horr kama chanzo kikuu cha mgawanyiko huo.

Aidha Makori amewataka wanasiasa kusita kutumia matamshi ya uchochezi wakti wa kuwasilisha lalama zao kwani zinaleta mgawanyiko zaidi.

Kadhalika amewataka vijana kutotumiwa na wanasiana kusababisha machafuko jimboni.

 

Subscribe to eNewsletter