County Updates, Local Bulletins

Shule ya upili ya wasichana ya Moi katika kaunti ya Marsabit yafungwa kwa muda usiojulikana.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya upili ya Moi Baada ya Shule hiyo kufungwa.
Picha Radio Jangwani.

Na Waihenya Isaac

Shule ya upili ya wasichana ya Moi katika kaunti ya Marsabit imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya bweni moja shuleni humo kuteketea usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa naibu mwalimu mkuu wa shule hiyo Bwana Festus Kiema ni kuwa uamuzi huo umeafikiwa baada ya bodi ya shule hiyo pamoja na wadau katika sekta ya elimu jimboni kukutana leo asubuhi.

Inaarifiwa kuwa moto na ambao chanzo chake hakijabainika hadi kufikia sasa, ulizuka katika bweli hilo la wanafunzi wa kitado cha pili mida ya saa kumi na moja na robo asubuhi, na kutekezeteza mali yenye dhamana iliyojulikana wakti wanafunzi wakiwa darasani.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya upili ya Moi Baada ya Shule hiyo kufungwa.
Picha Radio Jangwani.

Mwalimu Kiema ametaja kuwa hakuwa mwanafunzi yeyote alijeruhiwa wakati wa mkasa huo huku tayari uchunguzi ukianzishwa ili kubaini chanzo cha moto huo.

Wanafunzi wanatarajiwa kusalia manyumbani hadi usimamizi wa shule hiyo utakapotoa maelezo kuhusu siku ya kurejea shuleni.

Mabaki ya baadhi ya saduku za wanafunzi wa shule ya upili ya Moi Baada ya Shule ya bweni moja la shuleni humo kuteketea.
Picha Radio Jangwani.

Kisa hichi kinajiri siku tatu tu baada ya sehemu ya bweni moja kuteketezwa shuleni humo, kwa kile usimamizi wa shule hiyo ulichokitaja kuwa ni hitilafu za nguvu za umeme.

Hii ni shule ya pili ya upili kufungwa hapa jimboni Marsabit baada ya shule ya upili ya Laisamis kufungwa siku ya jumatatu baada ya wanafunzi kuaandaa mgomo na kuharibu mali ya shule kutokana na kile kilichokitajwa kuwa “wanafunzi hawataki kuamushwa asubuhi kusoma”.

 

 

 

 

Subscribe to eNewsletter