IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
By Adano Sharawe,
Shughuli ya kuwasajili makurutu wa kujiunga na kikosi cha jeshi, KDF imeendelea leo katika kaunti ya Marsabit eneo bunge la Sakuu, huku vijana wengi wakikosa nafasi ya kujiunga na kikosi hicho licha ya kuwa na vyeti vinavyohitajika.
Luteni Kanali Martin Maluki ambaye ndiye msimamizi wa zoezi hilo katika eneo la Sakuu amesema changamoto kubwa wamekubana nayo ni kutofautiana kwa majina kwa vyeti vyao.
Wanaume watatu kutoka Central, Dirib na Gadamoji walisajiliwa wakati wa zoezi hilo.
Nao vijana waliojitokeza kushiriki zoezi hilo wameeleza kufurahishwa na namna maafisa wa KDF walivyoendesha zoezi hilo kwa njia ya uwazi.
Wakati uo huo, wanawake wengi walijitokeza eneo bunge la Saku, lakini wakafamishwa kuwa KDF ilitaka wanaume pekee.
Baadhi ya wakazi waliokuwa wanashuhudia zoezi hilo lililofanyika katika shule ya Msingi ya Saku wameeleza kutoridhishwa kwao na hatua hiyo na wanalaumu serikali kwa kuwabagua wanawake. Abdirahman Somo amesema kuna haja ya kitengo cha jeshi kuwa na usawa wa kijinsia badala ya kuwapa kipaumbele wanaume pekee.
Hata hivyo, Luteni Kanali Maluki amesema baadhi ya maeneo nchini yana wanawake wengi ambao wanahudumia jeshi la Kenya KDF, hatua ambayo anadai ilichangia wanawake kufungiwa nje wakati wa shughuli ya usajili wa makurutu mwaka huu.
Zoezi hilo lilianza siku ya Jumatatu huko Dukana, siku ya Jumanne mijini North Horr na Moyale, siku ya Jumatano lilifanyika Loyangalani na Sololo, siku ya Alhamisi Turbi na Bubisa na siku ya Jumatatu itakuwa zamu ya wenyeji wa Laisamis.
Aidha, linatarajiwa kuendelea hadi tarehe 19 mwezi huu, ambapo maafisa wakuu wa KDF watasimamia usajili huo katika vituo mbali mbali vya kaunti ndogo zote kote nchini.