County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Serikali Kuwachukulia Hatua Kali Viongozi Waliohusika Katika Kupanga Na Kufadhili Mapigano Ya Kikabila Kaunti Ya Marsabit. – Asema Waziri Matiangi

By Adano Sharawe,

Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria viongozi waliohusika katika kupanga na kufadhili mapigano ya kikabila yaliyoshuhudiwa kaunti ya Marsabit.

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Dkt Fred Matiangi amesema serikali inaendelea kuwachunguza viongozi ambao wamekuwa wakiwapa silaha wenyeji kuiba mifugo na kutekeleza mauaji jimboni.

Akifika mbele ya Kamati ya Usalama wa taifa katika bunge Matiang’i amesema kuwa maafisa wa usalama watazindua operesheni kali ya kutwaa silaha haramu zilizoko mikononi mwa raia ili kuhakikisha ya kwamba usalama kamili unadumishwa.

Kauli yake inajiri baada ya visa vya utovu wa usalama kushuhudiwa katika sehemu za Halakhe Yahya na Turbi mwezi uliopita.

Subscribe to eNewsletter