County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Polisi Wamtia Mbaroni Mhalifu Mmoja Na Kufanikiwa Kuwarejesha Zaidi Ya Mifugo 29 Walioibiwa Katika Eneo La Mata Arba Hapa Jimboni Marsabit.

Baadhi Ya Mifugo Walioibiwa,Baada Ya Kuokolewa.
Picha;Hisani

By Mark Dida,

Idara ya polisi haitalegeza kamba Katika juhudi za kukabiliana na wezi wa mifugo hapa jimboni Marsabit.

Hayo ni kwa mujibu wa OCPD wa Marsabit ya kati Johnstone Wachira.

Wachira ameyataja hayo baada ya maafisa wa polisi kufanikiwa kuwarejesha zaidi ya mifugo 29 walioibiwa jana jioni katika eneo la Mata Arba  eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit na vilevile kumtia baroni mhalifu  mmoja.

Baadhi Ya Mifugo Walioibiwa,Baada Ya Kuokolewa.
Picha;Hisani

Wachira amesema kuwa idadi ya ngombe 7, ndama 5, pamoja na mbuzi 17 wamerejeshwa na polisi badaa ya makabiliano makali kati ya polisi na wahalifu hao.

Aidha Wachira ametoa uwito kwa wakaazi wa jimbo hili kupiga ripoti kuhusu wizi wa mifugo na kusaidia idara ya polisi wakti oparesheni inapoendelea.

Kadhalika Ali ambaye ni mwathiriwa ameweka wazi kuwa wahalifu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walivamia nyumbani kwake mida ya saa tisa usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kutoweka na mifugo hao.

 

Subscribe to eNewsletter