County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Oparesheni Ya Kuwasaka Wezi Wa Mifugo Walioibiwa Katika Eneo La Halakhe Yahya Inaendelea – Kamishna Paul Rotich

Picha:Hisani

By Mark Dida,

Kamishina kaunti ya Marsabit Paul Rotich amesema kuwa oparesheni ya wezi wa mifugo walioibiwa ktk eneo la Halakhe Yahya eneobunge la Saku inaendelea kwa siku ya pili na inatazamiwa kuzaa matunda baada ya polisi kuwatia mbaroni watu watatu katika eneo hilo.

Rotich aidha ameomba viongozi kutoka kaunti ya Marsabit kujitokeza na kusaidia idara ya usalama ili kufanikisha oparesheni hiyo.

Hata hivyo amesema kuwa idara ya usalama ipo tayari kuchukua hatua dhidi ya wale wanaozua uhasama na kuendeleza uhalifu katika kaunti ya Marsabit akiongeza kuwa mgogoro unaoshuhudiwa siku za hivi karibuni kati ya jamii ni uhasama wa kulipiza kizazi.

Picha; Hisani

Kwa upande yake mwakilishi wa wadi ya Sangete Jaldesa Sora Katelo ametoa wito kwa serikali kufanya upelezezi wao kupitia watu waliotiwa mbaroni walipokuwa kwenye gari siku ya jana.

Aidha amedokeza kuwa resiti iliopatikana katika eneo ya Bwawa ya Halake yahya itasaidia serikali kufanya uchunguzi wa haraka.

Wakti uo huo viogozi vya kutoka jamii wa Borana wameipa serikali siku mbili kufanikisha oparesheni hiyo.

Viogozi hao aidha wameelekeza kidole cha lawama kwa serikali kwa kulegeza kamba katika oparesheni ya kutafuta wahalifu.

Subscribe to eNewsletter