County Updates, Diocese of Marsabit

Ni Hatia Kukata Ua Wa Umeme Wa Shirika La KWS.

Picha;Hisani

By Mark Dida,

Naibu mkurugezi wa shirika la kulinda wanyama pori kws Katika eneo la kaskazini mwa kenya Robert Obrein amewasuta wafugaji kwa kukata ua wa umeme Katika eneo la hulahula na karare ili kupata njia ya mkato kuingia msitituni.

Akizungunza na idha hii kupitia njia ya simu Obrein ametaja kuwa hili huenda likasababaisha ndovu kupenya nje ya misitu.

Aidha Obrein ametaja kuwa  shirika la KWS litashirikiana na shirika la NRT kuweka ua mpya ili kuzuia  wanayapori kama vile ndovu kuingia katika mashamba ya wakulima.

Kadhalika  amewarai wakaazi wa jimbo hili kutunza ua huo na kuutaja kuwa wenye manufaa kwa  wakazi wa maeneo ya Kituruni na Songa  kwani kero la kusumbuliwa na wanayapori kama ilivyokuwa hapo awali halimo tena.

  

 

Subscribe to eNewsletter