County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Mwakilishi wadi wa Korr ataja ukosefu wa maji kuwa janga kuu hilo.

Mwakilishi wadi wa Korr/Ngurnit Daud Tomasot.

 

Na Samuel Kosgei,

Mwakilishi wadi wa Korr/Ngurnit Daud Tomasot ametaja kuwa hali ya ukosefu wa maji katika eneo la Korr kuwa janga kuu na kero sana katika hilo iwapo mvua haitanyeshi hivi karibuni.

Tomasot anasema kuwa licha ya visima vingi kuchimbwa maji mengi yanatopatikana ni ya chumvi hivyo kuwa vigumu kutumika na binadamu.

Anazidi kutoa wito kwa wafadhili kuingilia kati na kusaidia kuwapa mashine ya kutenganisha maji tamu na chumvi. Anasema sehemu nyingi wakaazi hutembea Zaidi ya kilomita 20 kusaka maji ya kunywa.

Aidha amewaomba wakaazi wa mji wa Korr kukubali ujio wa mabadaliko bila kuukata akitolea mfano kisa ambapo wakaazi wa mji huo waliwahi kumfurusha mwanakandarasi alikuwa na nia ya  kurekebisha kisima kikuu cha maji ambacho kingesuluhisha matatizo ya maji katika mji huo.

 

Subscribe to eNewsletter