County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Mtu Mmoja Auwawa Huku Mwingine Mmoja Akiuuguza Majeraha Ya Risasi Baada Ya Majambazi Kuvamia Eneo La Maji La Halakhe Yaya Hapa Marsabit Na Kuiba Mifugo.

Picha:Hisani

By Jillo Dida,

Mtu Mmoja Ameuwawa Huku Mwingine Mmoja Akiuuguza Majeraha Ya Risasi Baada Ya Majambazi Kuvamia Eneo La Maji La Halakhe Yaya Eneo Bunge La Saku Kaunti Hii Ya Marsabit Na Kuiba Mifugo Leo Asubuhi.

Akithibitisha Hayo Kamanda Wa Polisi Katika Kaunti Ya Marsabit Samuel Mutunga Amesema Kuwa Anayeuguza Majeraha Ni Mwanaume Mwenye Umri Wa Miaka 53 Huku Aliyeuwawa Akiwa Mwanaume Mwenye Umri Wa Miaka 31 Ambao Walikuwa Wakifuga Mifugo Yao.

Mutunga Aidha Amewaomba Viongozi Wa Kaunti Hii Kushirikiana Kwa Pamoja Ili Kutafuta Suluhu La Kudumu Katika Kutatua Mizozo Kati Ya Jamii.

Haya Yamejiri Huku Idadi Jumla Ya Mifugo Mifugo 323 Mbuzi Na Ngombe Wakiibiwa Hiyo Jana Katika Kisa Ambacho Pia Mtu Mmoja Aliuwawa Huku Mwingine Kujeruhiwa Katika Eneo La Turbi Eneo Bunge La North Horr.

Kulingana Na Ripoti Ya Polisi Ni Kuwa Leo Zaidi Ya Ngombe 300 Wameibiwa An Wajambazi Wasiojulikana.

 

Subscribe to eNewsletter