VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAMEITAKA JAMII KUZINGATIA MAADILI ILI KUEPUSHA VISA VYA MAUAJI VYA WANAWAKE NCHINI
November 5, 2024
By Jillo Dida Jillo,
Mbunge wa Moyale Qalicha Gufu ameiomba serikali na tume ya maridhiano ya kitaifa NCIC kumkamata na kumshtaki aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Torbi, Pius Yatani kwa kutoa matamshi ya uchochezi ya kijamii katika kaunti ya Marsabit miaka miwili iliyopita.
Mbunge huyo ameteta kuwa licha ya agizo la polisi kumkamata mwanasiasa huyo, bado hajatiwa mbaroni kutokana na kosa la kutoa matamshi ya uchochezi kutoka Ethiopia hadi Tana River dhidi ya Jamii Oromo.
Akizungumza na Radio Moja humu nchini, Gufu amemshutumu mwakilishi wadi huyo kwa kuchangia utovu wa usalama katika kaunti ya Marsabit,mzozo ambao umeshuhudiwa kwa muda mrefu.
Kauli hii inajiri siku chache baada ya waziri wa fedha Ukur Yattani ambaye ni mshirika wa karibu wa Pius kuwashitaki wanasiasa watatu kutoka kaunti za Marsabiti na Isiolo kwa kumchafulia sifa mwezi uliopita .
Ukur,kupitia kwa wakili wake G&A Advocates, amewataka mwakilishi wa wanawake wa Isiolo Rehema Dida Jaldesa, mbunge wa Saku Dido Ali Raso na Qalicho Gufu Wario wa Moyale kuomba msahama kwa kosa hilo .
Mbunge huyo pia amesema kuwa hakuna haja ya kuhofia kisa cha maajuzi ambapo bunduki moja ilipatikana ndani ya gari ya serikali ya kaunti ya Marsabit.
Aidha Kalicha amepongeza juhudi za MCA wa Uran Halkano Konso kujisalimisha katika afisi ya DCI kwa uchunguzi zaidi.
Kaunti ya Marsabit imeshuhudia utovu wa usalama wa mara kwa mara unaoletwa na makundi ya wezi wa mifugo waliojihami kwa silaha.