KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
By Samson Guyo,
Huku bajeti ya kitaifa ikitarajiwa kusomwa alhamisi tarehe 10 mwezi huu,baadhi ya wananchi katika kaunti ya Marsabit wameelezea kusikitishwa na baadhi ya maswala yaliyopo kwenye bajeti.
Wakizungumza na idhaa hii wakaazi hao wamelalama kuwa mwaka nenda mwaka rudi matatizo yamekua yale yale kwa wananchi wa kawaida.
Aidha baadhi yao wameelezea kuwa iwapo serikali itaweka mfumo kabambe kupigana na ufujaji wa mali ya umma pamoja na kupunguza madeni kutoka kwa nchi za nje basi bajeti ikitangazwa huenda fedha hizo zikamfaidi mwananchi.