County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Inter Faith Marsabit yakashifu vikali mauaji yanayoshuhudiwa hapa jimboni.

Baraza la madhehebu mbali mbali tawi la Marsabit likiwa kwenye kikao hapa mjini Marsabit.
Picha:Radio Jangwani

By Silvio Nagori,

Baraza la madhehebu mbali mbali tawi la Marsabit limekashifu vikali mauaji yanaendelea kushuhudiwa hapa jimboni.

Wakizungumza na waandishi wa habari hapa mjini Marsabit viongozi hao wamewataka wananchi kutolipiza kisasi jambo ambalo wamesema  kuwa linachangia katika vurugu za mara kwa mara.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Askofu wa jimbo katoliki la Marsabit Askofu Peter Kihara, viongozi hao wameitaka serikali kuongeza jitihada zaidi katika kuimarisha usalama na kuondoa silaha haramu miongoni mwa wananchi.

Mwanzo wa -Taarifa ya Baraza la madhehebu mbali mbali tawi la Marsabit.
Picha:Radio Jangwani

Aidha wamewataka wanasiasa kutowagawanya wananchi huku wakiwataka kuwapa hamasa  zaidi kuhusiana na umuhimu wa  Amani.

Vile vile hao wamekashifu matamshi ya chuki kati ya viongozi.

Mwisho wa -Taarifa ya Baraza la madhehebu mbali mbali tawi la Marsabit.
Picha:Radio Jangwani

 

Subscribe to eNewsletter