HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
By Samuel Kosgei,
Ni afueni kwa wakaazi wa kaunti ndogo ya Garbatulla baada ya serikali ya kaunti ya Isiolo kuzindua mashine aina tofauti ambazo zinalenga kuboresha huduma za matibabu katika eneo hilo na hata kwa watu wanoishi maeneo jirani.
Akizindua mashine hizo katika eneo la Garbatulla gavana wa kaunti hiyo Mohamed Kuti pamoja na wasimamizi wa sekta ya afya amesema kuwa sehemu ambazo kuna hospitali kuu ya umma katika kaunti hiyo itafaidika na mashine inayoitwa Telemedicine anayosema itasadia katika kuimarisha afya ya wakaazi wa kaunti hiyo.
Kuhusiana na usalama ambao umekuwa doda sugu kwa wakaazi wa eneo hilo, Gavana Kuti amekariri kuwa vituo vya polisi walizoahidi zitategenezwa ili kudhibiti mauaji ambayo nyingi yazo yamekua yakifanyika katika upande wa isiolo.