WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
By Isaac Waihenya.
Gavana Wa Kaunti Ya Marsabit Mahamoud Ali Amewataka Wananchi Kuzidi Kuzingatia Masharti Ya Covid Ili Kuzuia Msambao Wa Korona Katika Kaunti Hii.
Akizungumza Katika Hafla Ya Kufunga Mwaka Iliyoandaliwa Katika Makao Yake Hapa Mjini Marsabit,Gavana Ali Amewataka Wananchi Wakaunti Ya Marsabit Kuhakikisha Kuwa Wanafuata Maagizo Ya Wizara Ya Afya Ili Kupunguza Idadi Ya Maambukizi Jimboni Na Ambayo Tayari Imepelekea Serekali Yake Kupoteza Wafanyikazi Wawili.
Gavana Ali Vile Vile Ametaja Kuwa Mwaka Wa 2020 Uligubikwa Na Matatizo Mbalimbali Huku Jimbo La Marsabit Likiadhirika Pakubwa Kutokana Na Ukosefu Wa Amani, Nzige Wa Jangwani,Wizi Wa Mifugo Na Hata Janga La Korona Ambalo Limeyumbisha Ulimwengu Mzima.
Aidha Gavana Amesema Kuwa Licha Ya Changamoto Zilizokuwemo,Serekali Ya Kaunti Imepiga Hatua Kadha Ikiwemo Kuwafadhili Masomo Ya Wanafunzi Wanaofanya Vyema Jimboni.
Amewataka Wananchi Wa Marsabit Kusitisha Hulka Ya Umwagaji Damu Hapa Jimboni.
Kadhalika Mbunge Wa Saku Dido Ali Raso Ambaye Pia Alihudhuria Hafla Hiyo Amewataka Wananchi Kuishi Kwa Utengamano Bila Chuki Ya Ukabila.
Amesema Kuwa Wananchi Wanafaa Kudhamini Amani Katika Kaunti Hii Ili Kuwezesha Kaunti Hii Kushindana Na Kaunti Zingine Kimaendeleo.
Vilevile Jumbe Za Amani Zilisheheni Katika Hafla Hiyo Huku Wananchi Wakitakiwa Kuishi Kwa Amani Na Kutafuta Mbinu Salama Za Kusuluhisha Migogoro Inayojiri.