HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
By Waihenya Isaac
Bunge la Kaunti ya Marsabit limekuwa la hivi punde kupitisha mswaada wa marekebisho wa mwaka wa 2020.
Mswada huo wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa BBI umewasilishwa katika bunge hilo hii leo na kupitishwa na MaMCAs 24 bila kupingwa na yeyote.
Aidha ni MaMCAs 6 pekee waliokosa kuhudhuria kikao cha leo.
Awali, Bunge la Kaunti ya Marsabit lilikuwa limetoa nafasi kwa umma kutoa maoni yao kuhusu mswada huo kufikia hiyo jana.
Waliouga Mkono mswaada huo wametaja kuwa maswala ya mizozo ya mara kwa mara ambayo hushuhudiwa kila baada ya uchaguzi yatakuwa yakale.
VileVile wamesifia ongezeko la fedha kuelekea kwa majimbo huku wakitaja kuwa mandeleo zaidi yatashuhudiwa mashinani.
Tayari mswada huo umetimiza uungwaji mkono wa mabunge 24 yanayohitajika kikatiba ili uelekezwe katika Bunge la Kitaifa kujadiliwa.
Kufikia sasa Mabunge ya kaunti 32 yamepitisha mswaada huo Bunge la kaunti ya Baringo likiwa ndilo la kipekee kuupinga.