County Updates

Maafisa Wa shirika la Wanyama pori KWS Tawi La Marsabit wamewakamata wawindaji wawili haramu wakiwa na kilo 51.5 za Pembe Za Ndovu

Picha; Mark Dida.

By Mark Dida,

Maafisa Wa shirika la Wanyama pori KWS Tawi La Marsabit wamewakamata wawindaji wawili haramu wakiwa na kilo 51.5 za Pembe Za Ndovu katika eneo la Lag Malgis eneo bunge la Laisamis.

Wawili hao Wametiwa Mbaroni hii leo baada ya Maafisa Wa KWS kufanya upepelezi kwa muda wa miezi miwili.

Mkurugenzi wa shirika la KWS kanda ya kaskazini mashariki Robert Oburen akizungumza na wanahabari, amebaini kuwa wawili hao ni majangili sugu waliozoea kuwawinda wanyama pori kwa muda mrefu.

¸

Picha; Mark Dida

Robert amelitaja eneo la Lag Malgis kama eneo hatari kwa wanyamapori hasa ndovu kwani idadi kubwa wameuwawa katika eneo hilo.

Wawili hao wamepelekwa katika kituo cha polisi cha Marsabit wakisubiri kufikishwa mahakamani kesho.

Robert amesema Kuwa watazidisha msako dhidi ya wawindaji haramu jimboni huku akitoa tahadhari kwa wanaotelekeza uhalifu huo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa habari zozote kwa polisi ili kusaidia katika harakati zao za kuimarisha usalama wa wanyamapori jimboni.

Ameweka wazi kuwa wamepoteza ndovu 12 kwa muda wa mwaka mmoja, huku idadi ya ndovu katika msitu wa Marsabit ikipungua kutoka 177 mwaka wa 2017 hadi 165 mwaka 2020.

Subscribe to eNewsletter