County Updates

Afisa Mkuu Wa Mipango Ya Kiuchumi Kaunti Ya Marsabit Eng. Mohamed Tache Diba Atangaza Kuwa Ameambukizwa Korona

 Eng. Mohamed Tache Diba

Picha:Hisani

By Waihenya Isaac,

Afisa Mkuu Wa Mipango  Ya Kiuchumi  Katika Kaunti Ya Marsabit Eng. Mohamed Tache Diba Ameweka Wazi Kuwa Anaugua  Homa Hatari Ya Korona, Ingawa Hana Dalili Zozote.

Eng. Tache Ni Mmoja Kati Ya Watu 16 Kutoka Hapa Jimboni Waliokutwa Na Virusi Vya Korona Mnamo Siku Ya Jumapili Tarehe 29 Mwezi Jana.

Aidha Yeye Ni Baadhi Ya Wafanyakazi Wa Serekali Ya Kaunti Waliofanyiwa Vipimo  Mnamo Siku Ya Alhamisi Tarehe 26 Mwezi Jana.

Akizungumza Na Idhaa Hii Kwa Njia Simu,Tache Amebaini Kuwa Yu Salama Na Kuwa Anaendelea Na Matibabu.

Picha:Hisani

Tache Amewataka Wananchi Wa Jimbo Hilo Kuchukua Tahadhari Na Kujizuia Dhidi Ya Maambukizi.

Amewataka Kuzidi Kufuata Maagizo Ya Wizara Ya Afya Ya Kukaa Umbali Wa Mita Moja Unusu Na Pia Kuvalia Barakoa.

Wiki Jana Serekali Ya Kaunti Ya Marsabit  Kupitia Gavana Mohamed Ali Aliwataka Wafanyikazi Wote Wa Serekali Hiyo Kupimwa Virusi Vya Korona Baada Ya Aliyekuwa Katibu Wa Kaunti Eng. Joseph Wako Guyo Pamoja  Afisa Mkuu Katika Wizara Ya Fedha  Abdulahi Barako Kuaga Dunia Kutoka Na Ugonjwa Wa Covid 19.

 

Subscribe to eNewsletter