Wakaazi wa eneo la Arge,Marsabit walalamikia kile wamekitaja kuwa mnyama anayetisha…
February 24, 2025
Na JB Nateleng
Huku wanafunzi wakitarajiwa kurejea nyumbani kwa ajili ya mapumziko fupi ya muhula wa kwanza, wito umetolewa kwa wazazi kaunti ya Marsabit kuweza kuwa karibu na wanao ili kuwakuza kimaadili.
Akizungumza na idhaa hii, mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya SKM, Kame Koto amesema kuwa ni jukumu la wazazi kuwachunga watoto wanapokuwa nyumbani na kuhakikisha kuwa wanajua wanachofanya, ili kuwakuza kimaadili.
Kame ameelezea kuwa mtoto asipofuatiliwa kwa ukaribu basi huenda akaharibika kwa kujihusisha na mambo yasiyofaa.
Kadhalika mwalimu Kame amewataka wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao wanapata nafasi ya kudurusu wakati wa likizo hii fupi.
Aidha mwalimu Kame amewachangamoto pia viongozi wa kidini kuendelea kuwafunza watoto maadili mema ambayo yataboresha na kuimarisha imani yao.