Local Bulletins

Wananchi wamtakia Raila kila la heri katika uchaguzi wa AUC huku wengine wakiendelea kuonesha kukosa Imani na ufaulu wake.

NA JOSEPH MUCHAI

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wamemtakia aliyekuwa waziri mkuu humu nchini Raila Odinga kila la kheri kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa tume ya Afrika huku wengine wakipinga hatua hiyo na kupoteza imani kuwa Odinga atafaulu kutwaa nafasi hiyo.

Wakiongea na Radio Jangwani baadhi yao wanahisi kuwa kufaulu kwa Odinga kutakuwa na manufaa makubwa katika nchini ya Kenya haswa kimaendeleo.

Hata hivyo badhi wanahisi kuwa cheo hicho hakitakuwa na faida yoyote kwa taifa wakihoji kuwa Odinga amelazimishwa kuwania nafasi hiyo huku wengine wakihisi kuwa Odinga hana historia ya kufanya maendeleo.

Wakati uo huo Siku moja baada ya chama cha muungano wa Azimio la umoja one Kenya kuahidi kuwa Kitalemaza shughuli za bunge wakaazi Marsabit mjini wametoa maoni yao kuhusiana na swala hilo baadhi wakiunga mkono huku wengine wakikashifu hatua hiyo.

Miongoni mwa wale tulioongea nao mjini marsabit wanasema sio hatua nzuri kwa wabunge kulemaza shughuli hizo kwani sio jukumu lao kuamua anayefaa kuchukua nafasi ya walio wengi au wachache bungeni ila ni jukumu la waliotwikwa jukumu hilo kikatiba.

Haya yanajiri huku siasa za humu nchini zikionekana kuchukua mkondo tofauti kila uchao kutokana na mabadiliko katika sera na pia amri za mahakama.

Siku mbili zilizopita mbunge wa Suna East Junet Mohamed aliketi katika kiti cha kiongozi wa wengi bungeni kufuatia tamko la mahakama kuwa mrengo wa Kenya Kwanza sio wenye wabunge wengi bungeni ila ni upande wa Azimio la umoja one Kenya.

Subscribe to eNewsletter