Wakaazi wa eneo la Arge,Marsabit walalamikia kile wamekitaja kuwa mnyama anayetisha…
February 24, 2025
Na Samuel Kosgei
WAKAZI wa wadi ya Loglogo na Laisamis kaunti hii ya Marsabit wanazidi kutoa wito kwa idara ya afya jimboni kuzidisha juhudi kuzima kero la ugonjwa wa Kalaazar ambao wameutaja kuwa janga katika eneo hilo.
Wakaazi hao wakiongozwa na chifu wa Loglogo Andrew korole ameambia shajara kuwa hakuna mtu salama katika lokesheni yake kwani wanahofu ya kuagamizwa na Kalazar iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa na serikali.
Anasema japo idadi kubwa ya waathiriwa ni watoto kuna haja ya vifaa vya kupima, na dawa kufikishwa hospitalini kwa wingi.
Lesuan Leparleru ambaye mtoto wake aliathirika na ugonjwa huo ameitaka serikali kufanya zoezi la kunyinyiza dawa kwa manyatta zao ili kumaliza wadudu wanaoleta ugonjwa huo.
Wafanyabiashara pia wametajwa kuathirika kibiashara kutokana na uwepo wa ugonjwa huo vijijini na mjini.
Chifu amearifu kituo hiki kuwa kutokana na wageni kuogopa kupatana na wadudu hao hatari basi hali hiyo imewafanya wengi kukwepa mji huo wakati wa jioni.
Kauli yake imesisitizwa na Musa Lepurkei kutoka Loglogo anasema kuwa biashara haswa ya nyumba ya malazi imeathirika bila wateja.
Kulingana na afisa mtendaji wa hospitali ya kaunti ndogo ya Laisamis Liban Waqo ni kuwa hospiitali hiyo kufikia wikendi iliyopita wagonjwa 21 wametibiwa hospitalini na dawa na vifaa vya kupima vipo kufikia sasa.