WANACHAMA WA RANGELANDS SACCO WAPOKEA DIVIDENDS YA SHILLINGI MILLIONI SITA
February 20, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kushinikiza ongezeko katika fedha zinazoelekezwa katika maswala ya huduma za afya ya uzazi.
Kwa mujibu wa mshirikishi wa maswala ya haki za afya ya uzazi SRHR katika shirika la Faith to Action, Rebecca Mayabi, ni kuwa bajeti inayoelekezwa katika maswala ya afya ya uzazi imekuwa ikipunguzwa licha ya ongezeko la mahitaji mashinani kuongezeka maradufu.
Akizungumza wakati wa kufunguliwa kwa warsha ya siku tano, ya kuwapa mafunzo, vijana, mashirika ya kijamii pamoja na mashirika ya dini mbalimbali ni kuwa washikadau hawa wanafaa kuongea kwa sauti moja katika kuangazia maswala ya afya ya uzazi ambao yanaadhiri jamii ya Marsabit.
Aidha Mayabi amesema kwamba wamelenga kaunti ya Marsabit pamoja na kaunti za kaskazini mashariki kutokana na idadi ya juu ya visa vya mimba za mapema pamoja na ukeketaji ambavyo vinaripotiwa katika kaunti hizo.
Kwa upande wake mkurungenzi katika idara ya afya ya uzazi kaunti ya Marsabit Bi. Bokayo Arero amesisitiza hoja ya wazazi kuhakikisha kwamba wasichana waliokati ya umri wa miaka 12 hadi 15 wanapata chanjo ya HPV.