Local Bulletins

wakaazi jimboni Marsabit wametakiwa kusuluhisha mizozo ya kinyumbani kwa amani badala ya kuchukua sheria mikononi mwao

Na Caroline Waforo

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wapendanao dunia visa vya mauaji dhidi ya wanawake bado vinaendelea kushuhudiwa humu nchini.

Nyingi ya visa hivi vikiripotiwa kutekelezwa na watu walio kwenye mahusiano ya kimapenzi na wahasiriwa.

Kutokana na hayo wakaazi jimboni Marsabit na wananchi kwa ujumla wametakiwa kusuluhisha mizozo ya kinyumbani kwa amani badala ya kuchukua sheria mikononi mwao.

Ni wito ambao umetolewa na daktari wa afya ya akili katika kaunti ya Marsabit Dr Karani wakati wa hafla ya kutoa hamasa kwa wafungwa wa gereza la Marsabit.

Dr Karani ameambatanisha baadhi ya visa hivi na masongo wa mawazo.

Kutokana na hilo Dr Karani amewataka wananchi kutafuta msaada kutoka kwa wataalam wa afya wanapokabiliana na matatizo ya kiakili.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilionyesha kuwa kwa wastani, wanawake 47 wanauawa nchini Kenya kila wiki, wengi wao wakiuawa na watu wanaowafahamu.

Wapenzi, watu wa karibu wa familia na marafiki—watu wanaojulikana sana na wahasiriwa— wamekuwa wakigeuka wahalifu au kushukiwa katika visa vingi vya mauaji ya wanawake vinavyoripotiwa.

Subscribe to eNewsletter