WANACHAMA WA RANGELANDS SACCO WAPOKEA DIVIDENDS YA SHILLINGI MILLIONI SITA
February 20, 2025
Na Carol Waforo
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wapendanao duniani maarufu Valentine’s Day wananchi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwaonyesha upendo wafungwa na kukomesha unyanyapaa dhidi yao wanapokamilisha kifungo chao.
Ni wito ambao umetolewa na daktari wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Dr Victor Karani wakati wa hafla ya kutoa hamasa kwa wafungwa katika gereza la Marsabit hafla iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Open Mind Community Focus OMCF kwa ushirikiano na shirila la Equity afya, Redcross, kituo cha huduma Centre cha Marsabit pamoja na hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Dr Karani amewataka wananchi kuwaonyesha wafungwa hawa upendo ili kujihisi kukubalika tena miongoni mwa jamii.
Katika hafla hiyo Daktari Karani amewapa wosia wafungwa hao akiwataka kuzungumzia maswala yanayowasibu miongoni mwao au hata wafanyikazi magerezani kama njia mojawapo ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mwasisi wa shirika hilo la Open Mind Community Focus, Mariam Diba anasema uamuzi wa kuwatembelea wafungwa hao gerezani ni kuwaonyesha upendo wafungwa waliomo.
Ni katika hafla hiyo ambapo pia wafungwa hao wamepata fursa ya kupata mafunzo kuhusu njia mbalimbali za kukabiliana na msongo wa mawazo kama anavyoeleza Mariam.
Wafungwa hao wa kike na kiume walipokezwa zawadi mbali kama vile maziwa, sodo, sabuni kati ya zawadi nyingine.
Siku ya wapendanao huadhimishwa tarehe 14 mwezi February kila mwaka. Hii ni siku ambayo imetengwa kwa watu kuonyeshana upendo.