Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Joseph Muchai
Siku kadhaa baada ya mauaji ya watoto mapacha kuripotiwa katika eneo la Dukana eneobunge la North Horr imam wa msikiti wa jamia mjini Marsabit Sheikh Mohamed Noor amekemea kitendo hicho.
Akiongea na kituo hiki Sheikh Noor amesema kuwa ni kinyume na haki za binadamu na pia sheria za dini.
Wakati uo huo sheikh ameyataka mashirika ya kijamii kuingilia kati na kuwashirikisha jamii haswa walio mashinani kwenye mafunzo na hamasa ili kuepusha jamii na balaa kama hiyo.
Aidha noor amesema kuwa tukio hilo linarudisha watu nyuma kimaendeleo haswa ikizingatiwa kuwa jamii imepiga hatua muhimu kutoka kwenye mila potovu
Tukio hilo liliripotiwa mapema wiki hii ambapo wazazi wa watoto hao wanashukiwa kuwaua kwa kile kulingana na jamii wanamotokea kuwa na mapacha kama kifungua mimba huleta nuksi katika familia.