Vijana wa Saku wamelalamikia serekali ya kaunti ya Marsabit kutoidhinisha maswala waliyoibua wakati wa vikao vya kushirikisha umaa kwenye marekebisho ya bajeti…
February 5, 2025
Na JB Nateleng,
Vijana katika eneo la Saku wamelalamikia kutengwa na serekali ya kaunti kwa kukosa kuyaidhinisha maswala waliyoibua wakati wa vikao vya kushirikisha umaa (Public Participation) kwenye marekebisho ya bajeti ambayo yanadhamiria kufanyika wiki mbili zijazo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano wa manahodha wa mpira wa miguu eneo bunge la Saku Siba Burcha, vijana hao wamesema kuwa serekali inafaa kuipa maswala ya vijana kipaumbele ili kuwakwamua na kuwaendeleza mbele ili kuboresha maendeleo.
Burcha amewataka wawakilishi wadi kulipa kipaumbele swala la kuwahushisha vijana kupitia michezo akirai serekali kufadhali ligi itakayowapatanisha vijana katika kaunti ya Marsabit.
Aidha Burcha amesema kuwa japo wanahudhuria na kutoa maoni yao kwenye vikao vya kushirikisha umaa (Public Participation) bado masuala yao yanakosa kuangaziwa.
Kwa upande wake Halima Abdikadir ambaye ni Naibu karani wa Bunge la Vijana wa Saku (SYA) amesema kuwa kwa muda sasa serekali imeweza kuwatelekeza vijana jimboni hivi kufanya vijana kuweza kuingia katika matumizi ya mihadarati kwa sababu hawana kazi wala mahali pa kutegemea.
Kauli yake Halima ilimeungwa mkono na Rashid Abdi ambaye ni mwanachama wa Bunge la vijana wa Saku akisema kuwa ni jukumu la serekali kuweza kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya vijana jimboni.
Wakati uo huo, Hassan Mulata ambaye ni mratibu wa miradi katika shirika la Initiative for Progressive Change (IFPC) ameitaka serekali kulipa sikio kilio cha vijana na kutekeleza ipasavyo.