Local Bulletins

Valentines Day yasherehekewa kwa namna mbalimbali Marsabit.

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wamesherehekea siku ya wapendanao kwa njia mbalimbali.

Wakiongea na kituo hiki mjini Marsabit baadhi ya wakaazi wamesema kuwa siku hii ni spesheli sana tuu kwa wapenzi lakini pia kwa watu muhimu katika jamii. Hata hivyo wengi wao wanasema kuwa hali ya uchumi imesababisha wengi kutoisherehekea siku hii spesheli ya valentines.

Ni siku inayosherehekewa katika maeneo mengi duniani ambapo watu huzawadiana maua, kadi za mapenzi na zawadi nyingine muhimu kwa wanaowaenzi.

Wakati huo wanabiashara wanaojihusisha na bihdaa za zawadi za kimapenzi wanasema kuwa leo ndio siku yao muhimu kwani wateja wameongezeka kwa kiwango kikubwa.

Subscribe to eNewsletter