Raia 9 wa Eritrea na wawili Ethiopia wapigwa faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
February 24, 2025
Afisa mkuu anayesimamia maswala ya dharura kwenye sekta ya afya katika hosptali kuu ya ya rufaa Marsabit Abdi Sora amesema kuwa kampeni ya chanjo ya ugonjwa huo umezinduliwa leo katika hospitali kuu ya rufaa mjini Marsabit .
Uzinduzi huo ulijumuisha washikadau mbalimbali ikiwemo maafisa wa serikali kuu, serikali ya kaunti, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, WHO, UNICEF pamoja na wizara ya afya
Vile vile Abdi Sora amesema kuwa kampeni hiyo imezinduliwa kwa minajili ya kupambana na makali ya ugonjwa wa polio baada ya kisa kimoja kupatikana katika nchi jirani ya Ethiopia.
Kampeni hiyo ya OBR1 kulingana na Sora itaendelea kwa muda wa siku tano katika kaunti ya Marsabit pamoja na kaunti nyingine zilizopo karibu na nchi ya Ethiopia
Aidha Sora amesema kampeni hiyo inalenga watoto wenye chini ya umri wa miaka 11 huku shughuli za hamasisho zikiendelea kufanyika katika kaunti ya Marsabit.