Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Shirika la hifadhi ya jamii la Melako limepinga Taarifa zilizopeperushwa na runinga moja ya kimataifa kuhusu utumizi mbaya ya fedha za hewa ya Carbon (Carbon credit funds), ambayo shirika hilo limekisiwa kutumia vibaya pamoja na madai mengine.
Akizungumza na wanahabari kwa niaba ya Melako Community Conservancy, Joseph Lesoi amesema kuwa madai hayo si kweli na yanalenga kuharibu uhusiano mwema baina ya jamii na hifadhi hiyo.
Lesuloi amekariri kuwa hifadhi hiyo huwa inashirikiana na jamii katika kupanga miradi yake ambayo kwa muda sasa imeweza kuwanufaisha jamii zinaoishi katika maeneo ya Merille, Laisamis na Log Logo.
Lesuloi pia amekanusha madai kuwa walinzi wa hidhafi hiyo huwa wanawabaka wanawake katika eneo hilo akisema kuwa hakuna kisa chochote ambacho kimeweza kurekodiwa katika kituo cha polisi cha eneo hilo.
Lesuloi pia ameyakana madai ya kwamba walihusika katika kisa cha kutatanisha ambapo vyumba vya kuvutia watalii vileketea kwa njia ya kutatanisha.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa hifadhi ya jamii ya Melako, Simon Satim ni kwamba hifadhi hiyo haijahusika kwa vyovyote na madai yaliyoibuliwa ni ya uwongo kwa sababu lengo lao kuu ni kuboresha na kulinda rasilimali za jamii.
Satim ameelezea kuwa hifadhi hiyo imeweza kufadhili miradi mingi haswa ya kustawisha Amani kati ya jamii zinazoishi katika eneo la Marsabit kusini ambayo inajumuisha Merille, Laisamis Karare na Log logo.