WANACHAMA WA RANGELANDS SACCO WAPOKEA DIVIDENDS YA SHILLINGI MILLIONI SITA
February 20, 2025
Na Caroline Waforo,
Serikali ya kaunti ya Marsabit imeorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya kaunti 9 zilizotumia angalau asimilia 30 ya mgao wake kwenye miradi ya maendeleo katika mwaka wa kifedha wa 2023/24.
Hii ni katika ripoti aliyotolewa na hazina ya kitaifa.
Marsabit imeongoza katika orodha hiyo baada ya kuelekeza asimilia 38.6 ya mgao wake kwenye miradi ya maendeleo.
Kaunti ya pili ni Narok iliyotumia asilimia 34, ya tatu ni kaunti Homabay ambayo ilitumiwa asilimia 33.3.
Kaunti nyingine kwenye orodha hiyo ni pamoja na kaunti ya Mandera iliyotumia asilimia 33.3, Siaya asilimia 32.6, Transnzoia asilimia 31, Kitui asilimia 30.8, Kilifi asimilia 30.6 na kisha Turkana iliyotumia 30.6 katika mwaka huo wa kifedha.
Ripoti hiyo pia imeorodhesha kaunti 10 ambazo zilitumia chini ya asilimia 30 ya mgao wake kwenye miradi ya maendeleo.
Kaunti ya Nairobi ilitumia mgao wa chini zaid kwani ilitumia asilimia 10 tu ya mgao wake kwenye miradi ya maendeleo huku kaunti ya kisii ikitumia asilimia 13.7 kisha kaunti ya Mombasa ikitumia asilimia 16.2.
Kaunti nyingine zilizotumia mgao wa chini kwa maendeleo ni pamoja na kaunti ya Kisumu, Tiata Taveta, Kiambu, Kakamega, Vihiga, Nyamira na kisha kaunti Nandi.
Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa ni kaunti tatu nchini zilizotumia chini ya asilima 35 ya mgao wake katika kulipa mishahara na madeni. Kaunti hizo ni TanaRiver, Narok pamoja na Kilifi.
Kaunti zilizotumia fedha nyingi zaidi kulipa mishahara na madeni ni pamoja na kaunti ya Machakos iliyotumia asilimia 62.6, Kisii asimilia 61.1, Nandi asilimia 58.4 na Nairobi asilimia 58.
Kaunti zingine zilizotumia zaidi ya asilimia 50 ni pamoja na Embu, Nandi, Tharaka Nithi, Nyeri, Laikipia, Baringo, Lamu, Elgeiyo Marakwet, Muranga, Bomet, Kisumu, Kakamega pamoja na kaunti ya Bungoma.
Hii ina maana kuwa nyingi ya serikali za kaunti zilitumia fedha zake kulipa mishahara na madeni.
Kulingana na sheria ya usimamizi wa fedha za umma ya mwaka 2012 serikali za kaunti zinapaswa kutenga asilimia 30 ya bajeti kwa maendeleo.
Haya yanajiri huku wananchi katika kaunti ya Marsabit wakitoa maoni kinzani kuhusiana na ripoti hiyo iliyoorodhesha serikali ya Marsabit katika nafasi ya kwanza katika kutenga fedha za maendeleo
Baadhi ya wananchi tuliozungumza nao wanahoji kuwa hawajaona maendeleo inayotokana na kutengwa kwa fedha hizo.
Wakaazi hao wameitaka serikali ya kaunti ya Marsabit inayoongozwa na Gavana Mohamud Ali kufanikisha miradi ya maendeleo jimboni.
Aidha wengine wao wameipongeza serikali ya kaunti wakiisifia kwa miradi ya maendeleo humu jimboni.