Local Bulletins

Serekali kuu yaahidi kuwafidia wafugaji wa Marsabit, walipoteza mifugo kufuatia kiangazi kilichoshuhudiwa kati ya mwaka 2021 na 2023…

.“Sio lazima mradi upitie kwa wanasiasa ndio uwafaidishe wananchi”haya ni kwa mujibu wa kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau

Akizungumza hii leo wakati wa kikao cha kamati ya kutamidhimi majanga katika kaunti ya Marsabit (CSG) Kamau amesema kuwa kumekuweko na kasumba ya wanasiasa kuingilia miradi ambayo inanuia kusaidia jamii akisema kuwa hili lazima lisitishwa ili kuleta usawa katika ugavi wa rasilimali kwa wananchi wote.

Kamau amesema kuwa ni afueni iwapo miradi itawafikia wananchi wote kwa usawa na iwanufaishe badala ya kufikia kwa mtu mmoja na kukosesha jamii manufaa.

Matamshi yake Kamau yanajiri wakati ambapo serekali kuu ikishirikiana na serekali ya kaunti ya Marsabit kupitia idara ya mifugo inapanga kuanzisha mchakato wa kuweza kuwatambua wafugaji walipoteza mifugo kufuatia hali ya kiangazi iliyoshuhudiwa jimboni kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2023 ili kufanikisha mradi wa kutoa msaada wa mifugo.

Kamau ameelezea kuwa kufikia sasa bado idara ya mifugo jimboni haijapokea chanjo ya mifugo huku akisema kuwa bado wanashirikiana na serekali kuu ili kuweza kupata chanjo hiyo kwa ajili ya kuendeleza zoezi la kuwachanja mifugo jimboni.

Na huku idara ya mifugo nchini ikaendeleza mradi wa kutoa vifaa vya kuhifadhi maziwa maarufu (Milk Coolers) 230 katika kaunti 41 humu nchini, kamishina Kamau amesema kuwa kaunti ya Marsabit haikujumishwa kwenye mradi huu lakini kupitia ushirikiana na idara hiyo waliafikiana kuwa watajumuishwa katika awamu ya pili ya utoaji wa vifaa hivyo vya kuhifadhi maziwa.

 

Subscribe to eNewsletter