Gavana wa Marsabit Mohamud Ali apongeza rais Ruto kwa kuondoa hitaji la kupigwa msasa wakati wa kusaka kitambulisho….
February 6, 2025
NA ISAAC WAIHENYA
Ili tupunguze ndoa za mapema katika kaunti ya lazima kwanza tukabiliane na mila potovu ya ukeketaji.
Haya yamekaririwa na afisa mkuu katika idara ya jinsia kaunti ya Marsabit Anna Maria Denge.
Akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na ukeketaji nchini yaliyoandaliwa hapa mjini Marsabit, Anna Maria ametaja kwamba ukeketaji ndio huchangia ongezeko la mimba za utotoni sawa na ndoa za mapema hapa jimboni Marsabit.
Aidha Anna Maria ameweka wazi kuwa kwa sasa bado kuna jamii hapa jimboni Marsabit ambazo zinaendeleza miola potovu ya ukeketaji kwa asilimia 100 huku akiyataka mashirika yasiyo yakiserekali na washikadau wengine kushirikiana ili kupambana na hali hiyo.
Hata hivyo afisa mkuu huyu ameweka wazi kuwa wanashirikiana na wazee ili kuhakikisha kwamba wakomesha mila hii iliyopitwa na muda.
Kauli yake Anna Maria imeshanbikiwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la MWADO Nuria Golo, ambaye amesisitiza haja ya vikao kati ya idara ya jinsia, mashirika ya kijamii pamoja na wazee ili kufikisha kikomo kero hili la mila potovu ya ukeketaji.