Raia 9 wa Eritrea na wawili Ethiopia wapigwa faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
February 24, 2025
Na Isaac Waihenya,
Warsha ya siku tano, ya kuwapa mafunzo, vijana, mashirika ya kijamii pamoja na mashirika ya dini mbalimbali iliyolenga kuangazia maswala ya afya ya uzazi ambao yanaadhiri jamii ya Marsabit imekamilka hii leo.
Akizungumza baada ya kukamilka kwa hafla hiyo,mshirikishi wa maswala ya haki za afya ya uzazi SRHR katika shirika la Faith to Action, Rebacca Mayabi, amesema kuwa wamelenga kuangazia kuongezwa kwa bajeti haswa inayoelekezwa katika afya ya uzazi.
Mayabi amesema kuwa kwa sasa makundi hayo yamepewa maarifa ya kuweza kuendeleza mafunzo katika jamii mbalimbali vijijini.
Aidha mmoja wa walimu katika warsha hiyo Roselyn Pepela ameweka wazi kuwa warsha hiyo ilitoa hamasa kwa jamii kuhusiana na namna ya kufuatilia miradi inayoedeshwa vijijini ili kuhakikisha kwamba inaendana na mapendekezo yao.
Pepela ametoa wito kwa serekali ya kuaunti ya Marsabit kuwekeza zaidi katika kutoa hamasa kwa wananchi kuhusiana na maswala ya bajeti.
Hata hivyo baadhi ya wawakilishi wa mashirika mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, wamelipongeza shirika la Faith to Action kwa mafunzo hayo huku wakiahidi kuwa mabalozi mashinani na kuhakikisha kwamba haki za afya ya uzazi zinazingatiwa kikamilifu.