Gavana wa Marsabit Mohamud Ali apongeza rais Ruto kwa kuondoa hitaji la kupigwa msasa wakati wa kusaka kitambulisho….
February 6, 2025
NA JAMES MUCHAI
Mamake watoto mapacha walioripotiwa kuuawa katika manyatta ya Iliman Boru eneo la Dololo Boji katika kaunti ndogo ya North Horr anaendelea kuhifadhiwa katika makao salama ya Charity Sister Marsabit baada ya uchunguzi wa umri kudhibitisha kuwa hajafikisha umri wa miaka 18.
Kulingana na ripoti ya uchunguzi wa kimatibabu iliyowasilishwa mahakamani mnamo tarehe 4 mwezi Februari mwaka 2025 ilionyesha kuwa msichana huyo ana kati ya umri wa miaka 16-17.
Washukiwa wengine waliohusika katika kisa hicho ikiwemo mamake msichana huyo wanaendelea kuzuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.
Hakimu mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Simon Arome ameagiza kesi hiyo kutajwa tena tarehe 11 mwezi huu wa Februari.
Inakisiwa kuwa mapacha hao msichana na mvulana, waliuawa na wazazi wao kwa kunyimwa hewa pindi tu walipofika nyumbani baada ya kutoka hospitalini kutokana na Imani ya kitamaduni kuwa watoto wa kwanza mapacha katika jamii ya Gabra ni ishara ya laana kwa familia